Tukio hili ni hatua nyingine katika kuimarisha daraja la maelewano, ushirikiano na kuheshimiana baina ya mataifa mawili rafiki, likiwa pia kumbusho la wajibu wa kimataifa wa kusimama upande wa amani, maadili, na ustawi wa jamii.

Shirika la Habari la Kimataifa la Ahlul-Bayt (as) -ABNA- Balozi Mteule wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran nchini Tanzania, Mohammad Javad Hemmatpanah, ameweka historia mpya katika safari yake ya kidiplomasia baada ya kuwasili Ikulu Chamwino, Mkoani Dodoma, kwa ajili ya kuwasilisha Hati zake za Utambulisho kwa Mheshimiwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan, tarehe 11 Desemba 2025.

Mara baada ya kuwasili Ikulu, Balozi Hemmatpanah alipokelewa kwa heshima za kitaifa na kusaini Kitabu Maalum cha Wageni, ukiwa ni ishara ya kuanza rasmi muhula wake wa uwakilishi wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran hapa nchini.
Katika tukio hilo lenye umuhimu mkubwa wa kimataifa na kidiplomasia, pande zote mbili zimetumaini kuimarika zaidi kwa uhusiano wa kihistoria uliopo kati ya Tanzania na Iran, hususan katika maeneo ya elimu, afya, uchumi, nishati, utamaduni, na masuala ya kiulimwengu yanayohusu amani na haki za watu.

Tukio hili ni hatua nyingine katika kuimarisha daraja la maelewano, ushirikiano na kuheshimiana baina ya mataifa mawili rafiki, likiwa pia kumbusho la wajibu wa kimataifa wa kusimama upande wa amani, maadili, na ustawi wa jamii.

Mwisho kabisa, viongozi hao wanatarajiwa kuendeleza mazungumzo ya kina kuhusu ajenda mbalimbali za ushirikiano zinazolenga kuwanufaisha wananchi wa pande zote mbili.

Your Comment